Nabi awapeleka wachezaji Yanga ufukweni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2022
Nabi awapeleka wachezaji Yanga ufukweni

Kocha wa Yanga, Nasreddin Nabi, anapambana kutafuta stamina kwa wachezaji wake na kikosi hicho kitaendelea na mazoezi yake kwenye fukwe za Coco, Masaki jijini Dar es Salaam

Nabi amekiri kuwa hakupata muda mzuri wa kukiandaa kikosi chake kabla ya msimu kuanza hivyo atatumia muda huu ambao Ligi Kuu Bara imesimama kukisuka kikosi chake.

Alisema ratiba yake inabadilika kutokana na jinsi anavyowaona wachezaji wake baada ya mazoezi, huku akibadilisha aina ya programu yake baada ya kumaliza ya Gym wiki hii na sasa wamehamia ufukweni.

"Siku tatu nyuma nilidhani hatutorudi tena gym, lakini jana (juzi) asubuhi tulifanya mazoezi ya utimamu wa mwili jioni tulikuwa uwanjani na leo (jana) asubuhi tulikwenda ufukweni na jioni uwanjani," alisema kocha huyo

Alisema wachezaji wake wameanza kuelewana kwa kiasi fulani, lakini bado hawajafikia kiwango anachotaka hivyo ataendelea kuyafanyia kazi mapungufu ya kikosi chake.

Nabi alisema malengo yake ni kutetea ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2022/2023, Kombe la Shirikisho (FA) na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika michezo miwili ya mwanzo ya ligi, Yanga ilishinda 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania kabla ya kuwatandika Coastal Union 2-0.

Mchezo wa mzunguko wa tatu wa ligi, Yanga watacheza na Azam FC, Septemba 6, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 1.00 usiku

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’