Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amesema malengo yake msimu huu ni kuhakikisha anaibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC baada ya kuikosa tuzo hiyo msimu uliopita
Mayele tayari ameweka nyavuni mabao mawili msimu huu akifunga katika michezo yote miwili dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union
Amepachika mabao manne katika michezo mitatu, akifunga mabao mawili katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba
"Nashukuru nimeanza vizuri msimu huu nimefunga mabao mawili, msimu uliopita sikuweza kuwa mfungaji bora lakini msimu huu nitahakikisha nafasi vizuri zaidi ili niweze kufanikiwa," alisema Mayele
Msimu uliopita Mayele alifunga mabao 16 akizidiwa bao moja na mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole aliyepachika mabao 17
ADVERTISE HERE