Moloko kuiwahi Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Aug 2022
Moloko kuiwahi Azam Fc

Winga wa Yanga Jesus Moloko anaweza kurejea kikosini mapema kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Septemba 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Moloko alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union, mchezo uliopigwa mkoani Arusha

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema Moloko ameendelea kuimarika, matumaini ni makubwa ataiwahi Azam Fc

"Moloko anaendelea vizuri nafikiri anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wetu ujao kama mambo yataenda kama yalivyo sasa"

"Kuna umuhimu wachezaji kubadilika, nafahamu kila mchezaji anaipigania timu yake ishinde lakini hakuna uhusiano wa kukamia kumuumiza mwenzako," alisema Nabi

Katika mchezo dhidi ya Coastal Union ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, Moloko na Yannick Bangala walifanyiwa rafu mbaya ambazo zilipelekea kupata majeraha

Bangala aliweza kumaliza mchezo huo lakini Moloko alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Dickson Ambundo

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’