Tutawashambulia mwanzo mwisho - Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
10 Feb 2018
Tutawashambulia mwanzo mwisho - Lwandamina
Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, amesema hawatacheza soka la kujilinda katika mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St. Louis na badala yake watashambulia kuanzia dakika ya kwanza ili kumaliza mechi mapema.

Yanga jana ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Gymkhana tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa raundi ya awali utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lwandamina amesema kuwa wanataka kuutumia vyema uwanja wa nyumbani hivyo watacheza kwa tahadhari lakini ‘hawatapaki basi’ dhidi ya klabu hiyo kutoka Shelisheli.

“Tumewaona wapinzani wetu kupitia baadhi ya mikanda yao ya video, si timu mbaya, lakini lazima tuonyeshe kuwa tupo nyumbani, tutacheza soka la kushambulia lakini wakati huo huo tutakuwa makini kwenye kujilinda,” alisema Lwandamina.

Aliongeza kuwa anafahamu wapinzani wao watacheza soka la kujilinda kwa lengo la kuwabana ili wawe katika nafasi nzuri kwenye mchezo wa marudio utakaofanyika baada ya wiki mbili huko Shelisheli.

“Tutacheza kwa kasi zaidi dakika 15 za kwanza ili tupate bao la kuongoza, hii itatusaidia kushusha presha ya mchezo,” alisema.

Aidha, Kuelekea kwenye huo, Lwandamina, amepanga kuwatumia kwa pamoja washambuliaji, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa.

Ajibu ambaye amekosa baadhi ya michezo ya ligi kuu kutokana na kuwa majeruhi lakini sasa amepona na leo ataongoza safu ya ushambuliaji pamoja na Chirwa ambaye kwa sasa yupo kwenye kiwango cha juu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
58m ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →