Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati hakuna klabu inayoweza kuifikia Yanga kwa ukubwa
Arafat amesema wanakidhi vigezo vyote vilivyowekwa kushiriki michuano ya Africa Super League ambayo itaanza mwaka 2023
Katika mahojiano na chombo kimoja cha habari wakati akiwa ziarani nchini Uganda, Arafat alisema Yanga haiwezi kukosa usd Mil 1 kushiriki michuano hiyo
"Miezi sita iliyopita tulianza kuwasajili Wanachama wetu kidigitali, mpaka sasa tumeshasajili Wanachama 40,000 tukiingiza zaidi ya usd 500,000"
"Mpango mkakati wetu ni kusajili Wananchama Mil 1 na kukusanya zaidi ya Bil 24 kwa mwaka. Kwa ukubwa wetu hatuwezi kukosa fedha ili kushiriki Super League," alisema Arafat
ADVERTISE HERE