Baada ya Zalan Fc kuchagua kucheza mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa, Wananchi watacheza takribani dakika 360 katika uwanja huo
Septemba 06 Yanga itacheza na Azam Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu, Septemba 09-10 watacheza na Zalan Fc hapohapo kwa Mkapa katika mchezo wa mkondo wa kwanza ligi ya mabingwa, Yanga wakiwa wageni
Septemba 13 Wananchi watarejea tena katika uwanja huo kumenyana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Septemba 16-17 Wananchi watarejea tena uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakaribisha Zalan Fc katika mchezo wa marudiano michuano ya ligi ya mabingwa
Zitakuwa dakika 360 za burudani kwa Wananchi, malengo ni kushinda michezo yote minne
ADVERTISE HERE