Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania na Coasta Union
Nabi amesema licha ya kucheza mechi tatu katika kipindi cha siku saba, wachezaji wake wamejitoa na kuipambania jezi ya Yanga kuhakikisha wanashinda michezo yote
Juzi Yanga ilikamilisha mechi ya pili ligi kuu kwa kuichapa Coastal Union mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Yanga pia ilishinda mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza kwenye uwanja huo dhidi ya Polisi Tanzania
August 13 Yanga ilishinda mechi ya kwanza ya dabi dhidi ya Simba msimu huu wakitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Nabi alisema michezo miwili ya ligi waliyocheza mkoani Arusha ilikuwa migumu kutokana na kubanwa na ratiba
"Tumecheza mechi tatu katika siku saba, miili ya wachezaji ilichoka, uwanja pia haukuwa rafiki sana"
"Lakini nafurahi wachezaji wamejitambua na kujua umuhimu wa pointi tatu na umuhimu wa kila mechi ya ligi, tunaweza sema wamefanya kazi kubwa,” alisema Nabi
Yanga imerejea jijini Dar es salaam ambapo Nabi ametoa mapumziko kwa wachezaji wake kabla ya kuanza maandalizi ya mechi inayoifuata dhidi ya Azam Fc ambayo itapigwa Septemba 06 pamoja na mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Zalan ambao utapigwa Septemba 09-11 huko Sudan