Kuna watu wanachekelea baada ya kupewa ratiba ya kucheza dakika 270 mfululizo kwenye uwanja wa nyumbani wakati wenzao wakipewa dakika 180 za kibabe ugenini
Ni kama ulikuwa mtego kwa Wananchi ambao hata hivyo wameweza kuutegua baada ya kushinda mechi zote mbili
Mechi za raundi ya pili ligi kuu ya NBC zimekamilika jana Yanga ikiwa timu pekee iliyoshinda michezo yote miwili ugenini
Ni timu tatu tu zilizoshinda mechi zote mbili za mwanzo, Yanga, Simba na Singida Big Stars
Hata hivyo Simba na Singida Big Stars alama zao sita wamezikusanya katika viwanja vyao vya nyumbani
Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Azam Fc, utapigwa Septemba 06 katika dimba la Mkapa
Baada ya Azam, atakayefuata ni Mtibwa Sugar mechi hiyo pia itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Lakini kabla ya mchezo huo, Wananchi watasafiri nchini Sudan kuwafuata Zalan Fc kwenye mchezo wa kwanza hatua ya awali, michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika