Jana Afisa wa Habari wa Simba Haji Manara aliwaasa mashabiki wa timu yake kutoizomea Yanga kwenye mchezo wake wa ligi ya mabingwa dhidi ya St louis kesho Jumamosi.
Kauli hiyo iliwashangaza wengi na kuzua mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii wengi wakihoji kama kauli hiyo aliitoa kweli kutoka moyoni?
Leo Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga, Salum Mkemi aliijibu kauli hiyo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Makao Makuu ya klabu, Jangwani
Mkemi amesema kauli ya Manara ya kuwataka mashabiki wa Simba kutoizomea Yanga kesho haina maana kuwa mashabiki wa Yanga wakaishangilie Simba keshokutwa.
Mkemi amesema hilo haliwezekani 'abadan' kwa kuwa hakujawahi kuwa na urafiki wa aina hiyo baina ya timu hizo.
"Hatuwezi kuishangilia Simba,hili halitatokea, tulijaribu mwaka 93 lakini uzalendo ulitushinda!
"Hii ni kwa sababu hatujawahi na hatuwezi kuwa marafiki na wapinzani wetu, kwa hiyo naomba ieleweke wazi kuwa hatuwezi kuishangilia Simba kamwe."
Mwaka 1993 Simba ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika na kutandikwa mabao 2-0 na Stella Abdjan kwenye uwanja wa Uhuru.
Upinzani wa Yanga na Simba ni wa kihistoria. Sidhani kama kuna siku itatokea mashabiki wa timu hizo watashangilia timu pinzani.
Ni timu ya Taifa pekee ambayo huwaunganisha mashabiki wa Simba na Yanga.

ADVERTISE HERE