Mbona bado mapema sana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2022
Mbona bado mapema sana

Ukweli ni kwamba Yanga ilistahili kuondoka na ushindi mnono zaidi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao ulipigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapo jana

Yawezekana haikuwa siku nzuri kwa mwamuzi Ramadhan Kayoko aliyesimamia mchezo huo

Yapo matukio ambayo Yanga haikutendewa haki, kama Yanga isingepata ushindi jana pengine mjadala ungekuwa mkubwa sana siku ya leo

Mayele alifunga bao halali akipokea pasi kutoka kwa Heritier Makambo lakini katika hali ya kushangaza Kayoko alilikataa bao hilo na zaidi akampa Makambo kadi ya njano kwa tukio ambalo alimzidi nguvu mlinzi wa Polisi Tanzania aliyekuwa akiwania nae mpira

Matukio mengine ni pamoja na lile la Mayele kufanyiwa madhambi wakati akielekea langoni lakini yeye ndiye akapewa adhabu badala ya mlinzi wa Polisi Tanzania

Shuti la Bernard Morrison ambalo liligonga mwamba wa juu ni dhahiri mpira ulivuka mstari wa lango lakini mwamuzi 'akalipotezea' kabla ya Mwamnyeto kufunga bao la ushindi dakika chache baadae

Mapema kabla ya ligi kuanza, Bodi ya Ligi ilijipambanua kuwa msimu huu hawatarajii makosa mengi ya waamuzi kwani wamefanyia kazi changamoto hiyo

Lakini hali ni tofauti katika mchezo wa kwanza kabisa makosa yaleyale yaliyoonekna amsimu uliopita, yameanza kuonekana tena

Ni bahati mbaya zaidi kwa Yanga kwani wao wamekuwa wakiathiriwa sana na makosa haya yanayoitwa ya kibinadamu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’