Mazoezi ya Gym yapamba moto

Admin By Admin
β€’
15 Jul 2017
Mazoezi ya Gym yapamba moto
Wiki hii kocha wa Mkuu wa Yanga George Lwandamina amedhamiria kuimarisha miili ya wachezaji kwani wamekuwa wakifanya mazoezi makali ya Gym.

Kwa siku tatu mfululizo vijana wamekuwa wakipita 'tizi' la nguvu gym.

Mwanzo huu ni dalili nzuri kwa kikosi kwani mpaka msimu unaanza vijana watakuwa wameiva hasa.

Moja ya matatizo yaliyokuwa yanatukabili msimu uliopita ni wachezaji kuishiwa pumzi hasa kwenye dakika 30 za mwisho.

Tulishindwa kupata ushindi dhidi ya mahasimu wetu Simba sababu tu timu ilikuwa na matatizo ya kuishiwa pumzi kwente dakika za mwisho.

Tatizo hili Lwandamina amedhamiria kulimaliza, ameahidi kutengeneza timu yenye uwezo wa kucheza kitimu dakika zote bila ya kuwa na matatizo makubwa ya kuchoka.

Na hii ndiyo tofauti ya Lwandamina na Hans van Pluijm aliyekuwa kocha wetu kwa misimu miwili.

Pluijm wachezaji walimpenda sana kwa kuwa hakuwa 'akiwatesa' na mazoezi magumu walikuwa wakitumia muda mwingi kuchezea mpira.

Na ndio maana wakati wake Yanga ilikuwa ikicheza 'sexy football' tofauti alivyokuja Lwandamina.

Lakini mateso tuliyopata kwenye michuano ya Confederation hadi kuambulia ushindi katika mchezo mmoja kila mtu anajua.

Wapo wachezaji watakaochukia kutokana na mazoezi magumu anayotoa lakini mwisho wa siku wengi wanakiri ni kocha mzuri.

Akiwa na ZESCO mwaka juzi alifanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kutokana na uimara wa kikosi chake.

Aliunda kikosi ambacho kilikuwa hakifungiki kirahisi huku akitumia mfumo wa mashambulizi ya kushitukiza kupata ushindi.

Msimu wake wa kwanza na Yanga mwenyewe anasema haukuwa mzuri kwake kwa kuwa aliikuta timu ikiwa imeshajengwa na ikiwa katikati ya msimu pia.

Lakini sasa amedhamiria kujenga timu yake na ndio maana hata kwenye usajili ni yeye anayetoa kauli ya mwisho juu ya mchezaji gani asajiliwe.

Fahamuni Lwandamina anajenga Yanga ya Kimataifa.

Wakati upande ule wao wanatengeneza timu yao kutufunga, sisi tunatengeneza kikosi cha kushindana na timu kama TP Mazembe, Zamalek, El Ahly na Mamelod Sondowns kuwania ubingwa wa Afrika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
37m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’