Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema mlinda lango namba moja wa timu hiyo Djigui Diarra alipata majeraha katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba uliopigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Nabi huenda akampumzisha mdaka mishale huyo kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania, ambao utapigwa leo Jumanne kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Nabi amesema watamuangalia kwenye mazoezi ya mwisho yaliyofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Diarra aligongana na Pape Sakho katika mchezo huo ambao Yanga walitetea Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba
Hata hivyo Yanga haina presha yoyote kwenye eneo la mlinda lango kwani kama Diarra atakosekana, Aboutwalib Mshery atachukua nafasi yake
ADVERTISE HERE