Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza maboresho mbalimbali ya kanuni za ligi kuu ambazo zitatumika katika msimu huu wa 2022/23
Miongoni mwa kanuni zilizobadilishwa ni utaratibu wa kupata bingwa wa Ngao ya Jamii ambapo sasa timu nne zitachuana badala ya timu mbili utaratibu ulivyo sasa
Maboresho hayo yamebainisha kuwa kutakuwa na shindano la Kombe ka Ngao ya Jamii, ambapo timu tatu (3) za juu na Bingwa wa FA zitacheza mchuano huo maalum.
Endapo Bingwa yumo timu tatu za juu, basi ataingia anayeshika nafasi ya nne
ADVERTISE HERE