Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti kubwa waliyowapa wachezaji wao na kuhakikisha wanashinda dhidi ya Simba na kutwaa Ngao ya Jamii
Ulikuwa mchezo wa kwanza wa mashindano kwa Aziz Ki dhidi ya Simba, na kwa hakika moto uliuwasha kwelikweli
Aziz Ki alitoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Mayele na alikuwa mahiri kwenye kusambaza mipira hasa katika kipindi cha pili
"Namshukuru Mwenye ez Mungu, nawashukuru mashabiki wa Yanga, jana ilikuwa siku ya kipekee kwetu, tumefanikisha kile mlichohitaji, tunawashukuru kwa kutuunga mkono," alisema Aziz Ki
Ki alikuwa mwiba kwenye eneo la kiungo hasa baada ya kubadilishiwa majukumu katika kipindi cha pili akicheza namba 10
ADVERTISE HERE