Hatma ya Ngoma kujulikana wakati wowote

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Feb 2018
Hatma ya Ngoma kujulikana wakati wowote
Ratiba ya michezo iliyokaribu imepelekea Kamati ya utendaji kushindwa kuweka wazi hatma ya mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma ambaye ni majeruhi.

Hivi karibuni uongozi wa Yanga ulitoa taarifa juu ya kuitishwa kwa kikao ambacho kingemaliza sintofahamu ya mshambuliaji wake huyo raia wa Zimbabwe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema maamuzi juu ya swala la Ngoma yatawekwa hadharani wakati wowote.

"Ukaribu wa ratiba pamoja na kubanwa na majukumu kumepelekea kile ambacho kilipangwa kujadiliwa juu ya Ngoma kishindwe kufanyika," amesema Ten.

"Tuvumile, taarifa juu ya hatma yake itakuja baadae."

Ngoma amekosekana katika kikosi cha Yanga tangu mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka jana akikabiliwa na majeruhi.

Uongozi wa Yanga ulilazimika kumuagiza daktari wake kufanya uchunguzi wa afya ya mchezaji huyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’