Unbeaten inaendelea - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Aug 2022
Unbeaten inaendelea - Hersi

Kama ilivyokuwa msimu uliopita, jana Yanga ilihesabu taji la kwanza msimu huu kwa kuichapa Simba mabao 2-1 na kutetea Ngao ya Jamii

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema ushindi dhidi ya Simba ni mwanzo tu, wamedhamiria kuendeleza rekodi yao waliyoweka msimu uliopita kwa kutopoteza mchezo

"Tunashukuru kupata ushindi huu, umetuongezea morali kuelekea msimu mpya. Unbeaten inaendelea na safari hii itakuwa bora zaidi kuliko msimu uliopita," alitamba Hersi

Mabao mawili ya Fiston Mayele yalitosha kuihakikishia Yanga ushindi huo muhimu na kuwazima watani zao Simba ambao kabla ya mchezo walikuwa wakitamba kumaliza mchezo huo mapema

Walipofunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 16 presha ilikuwa kubwa kwa Yanga lakini mabadiliko aliyofanya Nabi kwenye kipindi cha pili kwa kuwaingiza Jesus Moloko na Bernard Morrison yalikuwa na faida kwa Yanga kwani nyota hao waliwapa wakati mgumu walinzi wa pembeni wa Simba na kuwafanya wasipande kama walivyofanya kwenye kipindi cha kwanza

Kama Mayele angekuwa makini pengine jana angekuwa mchezaji wa pili kufunga hat-trik kwenye mchezo wa dabi baada ya Abdallah Kibaden

Yanga sasa inahamishia nguvu zake kwene ligi ambapo kikosi kinaelekea Arusha kwa ajili ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa Jumanne August 16 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeui

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’