Pongezi nyingi kwa wachezaji wa Yanga na benchi la ufundi kwa kufanikiwa kuirejesha Ngao ya Jamii makabatini pale Jangwani kwa msimu wa pili mfululizo
Ulikuwa mchezo mgumu lakini hatimaye matokeo yamepatikana na furaha imeendelea kubaki Jangwani
Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri sana lakini Nabi amedhihirisha yeye ni master wa mbinu
Mmemuona Stephane Aziz Ki? huu ni mwanzo tu, Nabi huenda akalazimika kumbadilishia majukumu Fei Toto ili Aziz Ki atumike eneo la namba 10
Yanga inakuwa klabu ya kwanza kushinda Ngao ya Jamii mara saba wakiweka rekodi nyingine kama wanavyoongoza kwenye mataji ya ligi kuu
Hongera Wananchi, ulikuwa ushindi mzuri na wa heshima kwa Yanga
ADVERTISE HERE