Hili la kunyimwa uwanja halijakaa vizuri

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
9 Feb 2018
Hili la kunyimwa uwanja halijakaa vizuri
Tukio la jana la Yanga kuzuiwa kutumia uwanja wa Taifa kufanya mazoezi limemkera kocha Mkuu wa Mabingwa hao wa Tanzania Bara, George Lwandamina.

Lwandamina ameshangazwa na 'ukarimu' uliopitiliza kwa wageni wetu St Louis wakati kiuhalisia hali huwa tofauti tunapokwenda ugenini.

"Hawataki timu ifanye mazoezi Uwanja wa Taifa zaidi ya kucheza tu siku ile ya mechi, wakati wapinzani wetu wameruhusiwa kweli hii ni sawa?," alihoji Lwandamina

Moja ya silaha kubwa ya kupata mafanikio kwenye michuano ya Kimataifa ni kuhakikisha unashinda unapocheza kwenye uwanja wako wa nyumbani.

Hivyo mara nyingi timu mwenyeji huandaa mazingira ya kuhakikisha inaibuka na ushindi. Ushindi unaanza kutafutwa kihalali nje ya uwanja.

Mara ngapi tumeshuhudia timu zetu za Tanzania zinapokwenda kucheza hasa nchi za kiarabu huwa zinakosa hata usafiri wa kuwatoa uwanja wa Ndege?

Mara ngapi timu zetu huwa zinalazimika kubeba wapishi wa kuzipikia ugenini kwa kuwa vyakula vya wenyeji huwa vinaweka viungo vinavyoweza kuathiri afya za wachezaji?

Achilia mbali kugomea kuingia kwenye vyumba vya kupumzikia wakati wa mapumziko kwa kuwa vinakuwa vimepuliziwa dawa?

Niwaambie, moja ya sababu zinazopelekea nchi za waarabu kuwa juu kisoka barani Afrika ni kutokana na hizi figisu zao wanazofanya wanapokuwa nyumbani.

Huwa wanahakikisha wamekufunga kabla hujaingia dimbani kukumbana na vioo vya mashabiki vinavyomulika machoni muda wote wa mchezo!

Sasa kama hapa Tanzania timu mwenyeji inakatazwa jambo moja dogo tu la kutumia uwanja kwa ajili ya mazoezi huku mgeni akiruhusiwa basi kuna tatizo.

Sisi kama Taifa ina maana hatujali na hatuoni umuhimu wa timu zetu kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa.

Maana moja ya silaha za kufanya vizuri ni pamoja na maandalizi. Kocha alikuwa na program zake maalum ambazo alihitaji kuzifanya uwanjani kabla ya mchezo.

Kwa wale wanaosema kwamba ni sahihi kwa Yanga kuzuiwa kutumia uwanja wa Taifa kwa kuwa wanatakiwa kuwa na uwanja wao, sidhani kama wako sahihi.

Kama mgeni anaruhusiwa kutumia uwanja utakochezewa mechi kwa mujibu wa kanuni ili auzoee, kwa hiyo mwenyeji yeye haruhusiwa kuuzoea uwanja?

Ikumbukwe uwanja huo hautumiki mara kwa mara, unatumika kwenye baadhi ya mechi tu, hivyo huwezi kusema timu mwenyeji itakuwa imeuzoea.

Tena ingekuwa jambo jema kama TFF ingewezesha Yanga na Simba kutumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi wiki moja kabla ya michezo yao ya Kimataifa.

Ifahamike mafanikio ya Yanga kimataifa ni mafanikio ya Tanzania. Yule anayedhani anafanya maamuzi kuikomoa Yanga, basi ajue anaikomoa Tanzania
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’