Feisal Salum 'Fei Toto' ndiye aliyepeleka kilio mitaa ya Msimbazi kule jijini Mwanza kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) msimu uliopita
Leo Fei Toto atakuwepo dimba la Mkapa kuwawinda tena Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa kuanzia saa moja usiku
Ataungana na fundi mwingine Stephane Aziz Ki ambaye nae msimu uliopita aliwafunga Simba mabao mawili kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika
Bernard Morrisooooooon 'BM33' anaweza kuanzia winga ya kushoto huku Fiston Mayele akiwa mbele ya nyota wote watatu
Eneo la kiungo kazi ipo, kuna Gael Bigirimana na Khalid Aucho au Salum Abubakar 'Sure Boy'
Huku kwenye safu ya ulinzi nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto au Dickson Job huenda wakaanza na Yannick Bangala
Wakati walinzi wa pembeni Djuma Shabani na Kibwana Shomari au Joyce Lomalisa watakuwa na kazi maalum ya kupanda na kushuka
Langoni kama kawaida, mdaka mishale Djigui Diarra atakuwepo
kocha Nasreddine Nabi ana utajiri wa wachezaji bora kwenye kikosi chake, kazi ipo leo...!