Mayele....Makambo....Aziz...Morrisooon..oooh sisi ndio Yanga!, hivi ndivyo vibe la mashabiki wa Yanga litakavyokuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa leo katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba
Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na pengine Afrika nzima, utapigwa kuanzia saa 1 usiku
Yanga wataingia katika mchezo huo wakiwa ndio wanaoshikilia Ngao ya Jamii ambayo waliitwaa msimu uliopita kwa kuwafunga watani zao Simba bao 1-0
Kwa Yanga hakutakuwa na mabadiliko makubwa ya kikosi kwani Wananchi wameongeza nyota watano tu wakigeni
Wachezaji wapya waliosajiliwa ambao huenda leo watakuwa sehemu ya mchezo ni mlinzi wa kushoto Joyce Lomalisa, kiungo mkabaji Gael Bigirimana, kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki bila ya kumsahau winga hatari Bernard Morrison
Mshambuliaji Lazarus Kambole hatakuwa sehemu ya mchezo huo kwani bado hajapona majeraha aliyopata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc
Habari njema kwa Nabi ni kuwa leo ana uhuru wa kutumia wachezaji wote 11 wa kigeni ambao wako tayari kwa mchezo huo
Jana bodi ya ligi ilitangaza mabadiliko ya kanuni kuruhusu wachezaji wote 12 kutumika katika mchezo mmoja
Tukutane uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku....!