Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amesema wako tayari kuwapa furaha mashabiki wao kwa kushinda mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mwamnyeto amewaalika mashabiki wa Yanga wajitokeze kwa wingi dimba la Mkapa kwani wamewaandalia sapraisi ya aina yake
Mwamnyeto amesema mkakati wao ni kuhakikisha wanaifunga Simba ili kutetea Ngao ya Jamii ambayo waliitwaa msimu uliopita
ADVERTISE HERE