Kesho mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Simba utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga, mashabiki wameaswa kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha ule moto ambao Yanga ilimaliza nao msimu uliopita, wanaanza nao msimu huu
Ubora wa Yanga unatosha kuwapa jeuri Wananchi kuona wana nafasi kubwa ya kushinda Ngao ya Jamii kwa msimu wa pili mfululizo
Yanga haina mabadiliko makubwa ya kikosi ukilinganisha na watani zao, Simba
Ni wachezaji watano tu wageni kwenye kikosi cha Yanga, timu ni ileile ambayo msimu uliopita Simba walishindwa kuifunga bao lolote katika michezo minne ambayo timu hizo zilikutana
Ari ya wachezaji wa Yanga iko juu wakifahamu wanapaswa kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wao hasa baada ya kupoteza mchezo wa wiki ya Mwananchi dhidi ya Vipers Fc