Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amemaliza mkataba, nafasi yake iko wazi
Mwanahabari mkongwe Taji Liundi alikaimu majukumu ya Bumbuli katika shamrashamra za wiki ya Mwananchi na anapigiwa chapuo kukabidhiwa majukumu hayo
Bumbuli amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga tangu mwaka 2019 akichukua nafasi kutoka kwa Dismas Ten ambaye sasa ni CEO wa klabu ya Singida Big Stars
Leo Yanga imetangaza nafasi mbalimbali za kazi, nafisa ya Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ni miongoni mwa nafasi zilizotangazwa
ADVERTISE HERE