Kupitia Mkutano wake Mkuu wa Kawaida wa 44, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezindua mashindano mapya ya Africa Super League yatakayoshirikisha vilabu 24
Vilabu hivyo vitatoka katika kanda tatu za kisoka Afrika huku kila ukanda ukitoa vilabu nane vitakavyounda ligi hiyo itakayohusisha mataifa 16 barani kote
CAF imetaja sababu kuu ya kuanzisha mashindano hayo ni kukuza thamani ya mpira wa miguu Afrika kupitia uwekezaji, udhamini pamoja na mifuko ya maendeleo.
Africa Super League itachezwa kwa kipindi cha miezi 10 kuanzia Agosti hadi Mei kila mwaka na itakuwa na jumla ya michezo 197.
Fainali za mashindano hayo ambayo imepewa jina la SuperFinal itachezwa mwishoni mwa mwezi Mei katika dimba litakaloandaliwa kuwa na mfano wa fainali za SuperBowl (Marekani).
Katika mkutano huo, Rais wa CAF, Dkt. Patrick Motsepe amesema ndani ya miezi kadhaa ijayo, watatangaza mfumo mzima wa mashindano hayo na tarehe ambayo yatatarajiwa kuanza.