Yanga inakabiliwa na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi wakati huu inapoanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo kesho Jumamosi, Februari 10 2018 itashuka katika uwanja wa Taifa kuumana na St Louis ya Shelisheli kwenye mchezo wa kwanza hatua ya awali.
Hata hivyo baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi tayari wameanza mazoezi hivyo kurejesha matumaini ya Yanga kufanya vizuri.
Waliorejea ambao Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amethibitisha kuwa wako fiti kabisa ni Youthe Rostand, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vicent, Pato Ngonyani, Thabani Kamusoko na Ibrahim Ajib
Kurejea kwa wachezaji hao ni habari nzuri kwa kikosi cha Yanga ambacho kesho kimedhamiria kuifanya maangamizi St Louis pale uwanja wa Taifa.

ADVERTISE HERE