Winga wa Yanga Bernard Morrison amewataka mashabiki wa timu hiyo wasisikitishwe na matokeo ya kupoteza mchezo wa wiki ya Mwananchi kwani hayawezi kuwazuia katika malengo yao msimu
Morrison ambaye ametua Yanga akitokea klabu ya Simba, amewakumbusha Wananchi kilichotokea msimu uliopita katika wiki ya Mwananchi lakini wakafanikiwa kushinda mataji yote
"Nawakumbusha, mwaka jana mlipoteza mechi siku ya mwananchi, lakini mliendelea kushinda michezo yote mbele na kutwaa vikombe vyote nchini"
"Ilinisikitisha sana kiasi kwamba wakati mwingine nikienda kwenye kidimbwi na kuomba kikombe kwa ajili ya kinywaji changu, watasema ndugu yangu, Yanga imechukua vikombe vyote"
"Msiwe na huzuni kwa mchezo tuliopoteza kwa sababu mambo mazuri zaidi yanakuja. Ilikuwa nzuri kuwawakilisha tena. Asante kwa mapokezi mazuri jana," aliandika Morrison kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii