Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa Wiki ya Mwananchi ambayo kilele chake ni siku ya kesho Jumamosi, August 06 pale uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo watacheza na Vipers Fc
Nabi amesema kesho ni siku kubwa kwa Wanayanga wote nao wamejipanga kuifanya siku hiyo kuwa ya furaha zaidi
Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, Nabi amesema mchezo huo utawasaidia kuangalia kwa kiasi gani wachezaji wako tayari kwa ajili ya msimu mwingine wa mashindano
"Kesho ni siku kubwa, tumefanya maandalizi ya kutosha na tuko tayari kwa mchezo dhidi ya Vipers Fc. Tunawashukuru Vipers Fc kwa kukubali kucheza nasi katika siku hii"
"Mchezo utatusaidia kuangalia wachezaji wako tayari kwa kiasi gani kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii wiki ijayo. Matokeo ya ushindi yatakuwa mazuri kwetu ingawa muhimu zaidi ni kuangalia utayari wa timu yetu kuelekea msimu mpya," alisema Nabi
Aidha Nabi amebainisha kuwa wachezaji wawili Lazarus Kambole na Jesus Moloko walipata majeraha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc hapo jana, baada ya mazoezi ya mwisho leo watakuwa na uhakika kama wanaweza kutumika siku ya kesho au la
Yanga imekamilisha maandalizi yake mwisho kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo wakifanya mazoezi baada ya wapinzani wao Vipers Fc ambao nao waliruhusiwa kujifua katika dimba la Mkapa