Pitso Mosemano, Mkufunzi wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly, yuko Tanzania kwa mwaliko maalum kushuhudia kilele cha wiki ya Mwananchi
Akizungumza kwenye Mkutano na Wanahabari mapema leo, Mosimane amesema amefurahi kuja Tanzania kujifunza mambo mengine nje ya soka
Mosimane amesema kama mwafrika, anaunga mkono jambo jema linalofanywa na waafrika wenzake
Aidha Mosimane amesema alivutiwa zaidi ya 'parade' iliyofanywa na Yanga baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu
"Nilishangazwa na wingi wa mashabiki waliojitokeza kusherehekea ubingwa, ni tukio ambalo linaonyesha ni kwa kiasi gani Waafrika nasi tunaweza kufurahia matukio yetu"
"Yanga sio timu kubwa tu Tanzania, bali Afrika sote tunaifahamu. Najua mnaingia kwenye michuano ya CAF, najua mtafanya vizuri, kocha unapaswa kushinda mechi zote za nyumbani na kupata droo mbili ugenini inatosha. Nimekuwa katika mashindano hayo kwa miaka 12, nadhani inawezekana"
"Kwa sasa niko mapumziko, niliamua kusitisha mkataba wangu na Al Ahly, nilikuwa na mkataba wa miaka miwili lakini kwa sasa nahitaji kupumzika"
"Haikuwa rahisi mimi kuondoka Al Ahly lakini ilikuwa ni lazima niondoke nipate mapumziko, nimefanya kazi hii kwa miaka 21 pasipo mapumziko," alisema Mosimane