Yanga yazuiwa kufanya mazoezi uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Feb 2018
Yanga yazuiwa kufanya mazoezi uwanja wa Taifa
Kikosi cha Yanga leo asubuhi kililazimika kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Polisi jijini Dar es salaam baada ya kuzuiwa kutumia uwanja wa Taifa.

Yanga itatumia uwanja wa Taifa kwenye mchezo wake wa keshokutwa wa ligi ya mabingwa dhidi ya St Louis.

Lakini cha kushangaza Meneja wa uwanja huo amezuia Yanga wasiutumie kwa mazoezi huku akiwaruhusu wageni St Louis wautumie.

Kwa mujibu wa kanuni, St Louis wanaruhusiwa kuutumia uwanja utakaotumika katika mchezo dhidi ya wenyeji siku moja kabla ya mchezo husika.

"Huu sio uwanja wa mazoezi ni uwanja kwa ajili ya mechi, lakini kwa kuwa mgeni hajawahi kuutumia kanuni zinasema ni lazima wapate muda wa kufanya mazoezi kabla ya muda wa mechi," amesema Meneja uwanja wa Taifa.

Hiki ni kituko! Kwamba mwenyeji hana haki ya kutumia uwanja wa Taifa lake eti haukujengwa kwa ajili ya kufanyia mazoezi!

Ni ajabu kuona Yanga imekuwa ikikumbwa na vikwazo kila inapojaribu kutumia uwanja wa Taifa hasa baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa.

Kwenye ligi Yanga imetumia uwanja huo mara moja tu tena ikiwa mgeni kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

Katibu Mkuu Charles Mkwasa aliwahi kuhoji kwa nini Yanga imekuwa haipewi nafasi kutumia uwanja huo kama ilivyo kwa timu nyingine?
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’