Baada ya kurejea nchini na siku ya jana kuongeza mikataba yao, wachezaji Yannick Bangala na Djuma Shabani wameanza mazoezi na wenzao Avic Town
Nyota hao walichelewa kurejea kutokana na masuala ya kifamilia, kama ilivyo kwa winga Bernard Morrison ambaye anatarajiwa kuwasili usiku wa leo
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amethibitisha kuwa Morrison yuko njiani na anatarajiwa kutua nchini usiku na moja kwa moja kuungana na wenzake Avic Town
Aidha wachezaji saba ambao wako katika majukumu ya timu ya Taifa, nao wataingia kambini baada ya mchezo dhidi ya Somalia
ADVERTISE HERE