Nkane atamba, makombe hayataondoka Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jul 2022
Nkane atamba, makombe hayataondoka Jangwani

Winga wa Yanga Denis Nkane amesema wamepania kuhakikisha wanachukua vikombe vyote kwa mara nyingine

Akizungumza akiwa kambini Kigamboni ambako kikosi cha Yanga kimeweka kambi, Nkane amesema wao kama wachezaji wanaendelea vizuri na mazoezi ya fiziki na kuuchezea mpira, lengo ni kufanya vema msimu ujao kuwafurahisha wanachama na mashabiki wa Yanga

"Kambi inakwenda vizuri, tunafanya mazoezi yote ya kuweka mwili sawa na kuuchezea mpira. Msimu ujao naamini kama mchezaji nina deni kubwa kwenye michuano ya ndani na nje ya nchi"

"Naamini hili litafanyika nikiwa na ushirikiano na wachezaji wenzangu, tumejipanga kuchukua tena mataji yote matatu, ni kitu kinachowezekana kabisa na kama vingine vitaongezeka navyo tutavichukua," alisema Nkane

Alisema kuwa amejifunza vitu kadhaa kutoka kwa wachezaji Stephane Aziz Ki na Gael Bigirimana, kwa sababu ni wachezaji wakubwa na wameshacheza michuano mbalimbali mikubwa kuliko yeye.

"Nimefurahi na najivunia kucheza nao kwa sababu ni wachezaji wakubwa na mimi najifunza vitu kadhaa kutoka kwao, naamini muda utaongea na wanachama na mashabiki wa Yanga watafurahi"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’