Wakiwa wanaendelea na pre-season Avic Town, kikosi cha Yanga leo kilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp
Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 ambapo Fiston Mayele aliweka kambani mabao matatu 'hat-trik'
Mabao mengine yalifungwa na Stephane Aziz Ki na Heritier Makambo
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ametaka vijana wake wapate michezo mitatu ya kirafiki kabla ya mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi ambao utapigwa August 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE