Jana Yanga iliachia jezi zitakazotumika msimu ujao wa mashindanio, 2022/23
Wananchi wanaendelea kupigana vikumbo madukani kila mmoja akijipatia uzi wake mapema kuelekea Wiki ya Mwananchi ambayo shamrashamra zitaanza Jumatatu
Jezi toleo la tatu (nyeusi) imeonekana kubamba zaidi kwani ndio inayonunuliwa kwa wingi katika utafiti tuliofanya katika maduka kadhaa
Aidha jezi ya kijani inafuatia kwa kununuliwa ikiwa haijaachana sana na jezi ya njano
Mwitikio ni mkubwa sana, Wananchi walisubiri ujio wa jezi hizi na kwa hakika wengi wameridhika na ubora wake



ADVERTISE HERE