Kocha wa St Louis, Michel Renald amesema hakuna anachojua juu ya wapinzani wake hivyo anaamini mechi itakuwa ngumu.
"Ni mara yetu ya kwanza kuja hapa, hatujawahi kuja japa, Yanga wenyewe tumewajulia kupitia mtandao wa CAF.
"Hivyo mchezo utakuwa mgumu kwa sababu sizani kama wao wenyewe wanatufahamu sisi, "alisema.
Akizungumzia kuhusu kutuma wawakilishi katika mchezo wa Yanga dhidi ya Njombe Mji, alisema hana uhakika na suala hilo ila alipata taarifa ya ushindi wa wapinzani wao hao ambao watakipiga nao siku ya Jumamosi.
"Sisi tumeingia hapa usiku sana(Jumanne) hatukuweza kuiona hiyo mechi, lakini tulipata matokeo ya wapinzani wetu kwamba wameshinda, wamefanya vizuri kupata ushindi na sisi ndio tunaendelea na mazoezi, "alisema.
Hii ni mara ya tano kwa St Louis kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa. Mafanikio makubwa iliyopata kwenye michuano hiyo ni kufika raundi ya pili mwaka 2001.
Ni tofauti na Yanga ambayo imekuwa ikishiriki karibu kila mwaka na ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi mwaka 1998 huku mwaka 2015 ikitinga hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kutolewa kwenye raundi ya tatu, ligi ya mabingwa.
Hata hivyo Yanga itafanya makosa makubwa kama itawadharau wapinzani wao kwa kuwa tu hawafahamiki.

ADVERTISE HERE