Kabwili yuko tayari kuibeba Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Feb 2018
Kabwili yuko tayari kuibeba Yanga
Moja ya faida kubwa iliyopata Yanga msimu huu ni kuwa na kikosi chenye vijana wengi.

Licha ya changamoto ya majeruhi, Yanga imeendelea kufanya vizuri kutokana na upana wa kikosi chake.

Mmoja wa vijana hao ni mlinda lango Ramadhani Kabwili.

Uwezo wa Kabwili langoni ambaye ndio kwanza ametimiza miaka 18 umewashangaza wengi.

Tayari amedaka dakika 165 katika kikosi cha Yanga (dakika 75 dhidi ya Lipuli na dakika 90 dhidi ya Njombe Mji) kwenye michezo ya ligi kuu ya Vodacom.

Kabwili alianza kun'gara kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu, michuano ambayo Yanga ilitolewa kwenye hatua ya nusu fainali.

Wakati Yanga inamsajili kinda huyu ilikuwa kwa ajili ya kumkuza na pia kumtumia kwa dharura pale walinda mlango wake Youthe Rostand na Benno Kakolanya wakiwa majeruhi.

Lakini hilo huenda likawa limebadilika hasa baada ya kuumia kwa walinda lango hao namba moja.

Kwa uwezo ulio-onyesha Kabwili huenda 'majeruhi' hao wakajikuta wanaendelea kukaa benchi hata pale watakapokuwa timilifu.

Kabwili anashabihiana sana na mlinda lango mkongwe Juma Kaseja ambaye naye alianza kun'gara kwenye kikosi cha Simba akiwa na miaka 18 tu mwishoni mwa miaka ya 90.

Akiendelea hivi, ni swala la muda tu, atakamilisha ndoto zake za kwenda kusakata kabumbu katika ligi maarufu barani Ulaya
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’