Klabu ya Yanga leo imesaini mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya Sportpesa ambao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo iliyofanyika mapema leo katika Hoteli ya Johari Rotana, Mkurugenzi wa Utawala Sportpesa Abas Tarimba alisema mkataba huo una thamani ya Tsh Bilioni 12.335
"Hii ni historia kwa klabu ya Yanga kwani kwenye mkataba wa awali, thamani ya mkataba kwa miaka yote mitano ilikuwa Tsh Bil 5.2, Bil 1 kwa mwaka lakini sasa Yanga itavuna zaidi ya Tsh Bilioni 4 kwa mwaka," alisema Tarimba
Aidha Yanga itapata bonasi ya Tsh Milioni 150 kama itatwaa ubingwa wa ligi kuu na bonasi ya Tsh Milioni 112 kama watatwaa taji la FA na Milioni 75 kama watatinga fainali ya FA
Sportpesa pia leo wameikabidhi Yanga bonas ya Tsh Milioni 100 baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu