Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa awali wa ligi ya mabingwa dhidi ya St Louis.
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumamosi kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mkwasa amesema anayo taarifa kuwa St Louis wamewasili nchini kimyakimya tangu juzi, aina ya ujio wao huo hauitishi Yanga.
"Taarifa tulizonazo ni kuwa tayari wapinzani wetu wameshaingia nchini, wamewasili jana (juzi) usiku na wamefikia hoteli moja iliyoko maeneo ya Kariakoo, kwa upande wetu tunaendelea kujipanga kuhakikisha tunavuna matokeo mazuri," amema Mkwasa.
Katibu huyo aliongeza kuwa waamuzi wa mchezo huo ambao ni Belay Tadesse Assenese, Tigle Gizan Belachew na Kinfe Yilma Kinfe kutoka Ethiopia na kamisaa Frans Vatileni Mbidi wa Namibia, watawasili nchini leo.
"Tiketi za waamuzi na kamisaa tumeshatuma na tutawapokea siku moja kabla ya mechi, tunamuomba Mungu mambo yaende kama tulivyotarajia, tunajua mashindano ya kimataifa ni magumu kuanzia mechi ya kwanza, hakuna timu ndogo, lolote linaweza kutokea ndani ya dakika 90," alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga.
Baada ya mchezo huo wa kimataifa, Yanga itaendelea na mbio zake za kutetea ubingwa kwa kuwakaribisha Majimaji kutoka Songea katika mchezo utakaopigwa Februari 14, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru.

ADVERTISE HERE