Klabu ya Yanga inajipanga kumuongeza mkataba mshambuliaji wao kinara Fiston Mayele raia wa DR Congo, imefahamika
Mayele amebakisha mwaka mmoja akiwa tayari ametumikia nusu ya mkataba wa miaka miwili aliosaini wakati akisajiliwa na Yanga msimu uliopita
Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu Mayele katika dirisha hili la usajili akitajwa kuhitajika na klabu ya Kaizer Chiefs Yanga wakigoma kumuuza kutokana na mipango waliyonayo kuelekea msimu ujao
Sasa Yanga inataka kumuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ambapo wataboresha maslahi yake
Mayele anatarajiwa kurejea leo na moja kwa moja kuelekea Avic Town kuungana na wenzake ambao tayari wameanza pre-season
Wachezaji wengine ambao wanatarajiwa kuwasili leo ni Djuma Shabani, Yannick Bangala na Bernard Morrison