Winga wa Yanga Jesus Moloko anatarajiwa kuwasili nchini leo na moja kwa moja kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2022/23
Nyota wanaotoka nje ya nchi wamepewa mpaka siku ya Jumapili kuwa wamerejea na kuungana na wenzao wa ndani ambao tayari wako Avic Town
Wachezaji wengine kutoka DR Congo Djuma Shabani, Yannick Bangala na Fiston Mayele wanatarajiwa kuwasili Jumamosi
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mpaka kufikia Jumapili, wachezaji wote pamoja na benchi la ufundi watakuwa Avic Town
Wachezaji 19 wataanza pre-season, wachezaji wengine nane ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa, watajiunga na wenzao wiki ijayo
ADVERTISE HERE