Winga wa Yanga Bernard Morrison amepania kuwaziba midomo wale wanaomponda baada ya kuhamia klabu ya Yanga
Morrison amesema wakati yuko mapumziko alikuwa akifanya mazoezi makali tayari kwa msimu mwingine wa mashindano akiwaahidi Wananchi furaha
Pamoja na kuisaidia sana Simba hasa kwenye michuano ya Kimataifa msimu uliiopita, ni kama mchango wake hauonekani kuwa na thamani waajiri wake hao wa zamani wakimnanga kuwa mtovu wa nidhamu na hakuwa na msaada kwa timu hiyo
Morrison amesema, amepania kuja kivingine msimu ujao huku akiwatahadharisha wale watakaokutana nae uwanjani, wajipange
"Nilipata muda mzuri wa kufanya mazoezi wakati nikiwa likizo, niko tayari kucheza hata kesho. Naamini kama kocha atanipa nafasi ya kucheza mechi zijazo, nawaambia mtamuona Morrison mwingine kabisa," alisema Morrison
Yanga imeingia kambini leo kuanza maandalizi ya msimu mpya