Uongozi wa klabu ya Yanga umepokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) dhidi ya Msemaji wake ndugu Haji Manara
Kamati ya Maadili ya TFF leo tarehe 21 Julai imetangaza kumfungia ndugu Haji Manara kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya Shilingi za Kitanzania Milioni 20
Katika taarifa iliyotolewa na Yanga, imebainisha kuwa mabingwa hao wa Tanzania wanaamini Manara hakutendewa haki kwa adhabu hiyo kubwa hivyo Yanga inamuunga mkono katika kudai haki yake katika vyombo vya juu zaidi vya Kimamlaka

ADVERTISE HERE