Kinatoka chuma, kinaingia chuma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jul 2022
Kinatoka chuma, kinaingia chuma

Kwa hakika Wananchi wataendelea kuikumbuka kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji Yacouba Songne hasa katika msimu wake wa kwanza 2020/21

Katika msimu huo Yacouba aliibuka kuwa mfungaji bora wa kikosi cha Yanga akifunga mabao nane huku akitoa pasi za mabao sita katika msimu ambao Yanga haikuweza kufikia malengo yake

Msimu wa 2021/22 haukuwa mzuri sana kwa Yacouba kwani mwezi Novemba 2021 alipata majeraha makubwa ambayo yalimfanya asionekane tena uwanjani hadi msimu ukamalizika

Juzi Yanga imewataarifa Wanachama na Mashabiki wao kuwa Yacouba hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao

Yanga itazungumza na Yacouba kuona ni namna gani wanaendelea kumsaidia wakati huu akiendelea kuimarika baada ya majeraha ambayo yalimlazimu kwenda kutibiwa nchini Tunisia

Wakati nyota huyo kutoka Burkina Faso akitoka, anaingia nyota mwingine kutoka Burkina Faso Stephen Aziz Ki

Hii tunasema 'kimetoka chuma lakini kimeingia chuma kwelikweli'. Aziz Ki ndio usajili ghali zaidi uliofanywa katika ligi kuu ya NBC mpaka sasa

Aziz Ki amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikitumiwa na Yacouba

Wananchi watarajie kuanza kumuona Aziz Ki katika viunga vya Avic Town baadae leo, Wananchi wakianza kambi ya maandalizi ya msimu mpya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’