Wachezaji wa Yanga leo wanaingia kambini tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu, kombe la FA na michuano ya ligi ya mabingwa 2022/23
Siku ya kesho Alhamisi, Julai 21 Yanga itaanza rasmi maandalizi pale Avic Town
Yanga ina wiki mbili za maandalizi kuelekea Tamasha la Wiki ya Mwananchi ambapo kilele chake ni August 06, 2022
Aidha Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amepata wiki tatu za kukiandaa kikosi chake kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa August 13
Nabi ndiye aliyependekeza vijana wake kubaki Avic Town, akiamini wiki tatu zitatosha kukiweka sawa kikosi chake tayari kwa msimu mwingine wa mafanikio
ADVERTISE HERE