Yanga kuweka Pre-season Avic Town

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jul 2022
Yanga kuweka Pre-season Avic Town

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza rasmi kuwa maandalizi ya msimu mpya pre-season, yataanza Alhamisi Julai 21, Avic Town Kigamboni

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema uamuzi wa kuweka pre-season jijini Dar es salaam umezingatia mapendekezo ya benchi la ufundi

Manara amesema wachezaji pamoja na benchi la ufundi wataingia kambini Avic siku ya kesho Jumatano, Julai 20

"Tulikuwa na msimu mrefu, hivyo ilikuwa muhimu kwa wachezaji wetu kupata muda wa mapumziko, ni haki yao. Hivyo tunatangaza rasmi kuwa pre-season yetu tutafanya jijini Dar es salaam, Avic Town"

"Tuna vifaa vyote tunavyohitaji kwa ajili ya pre-season tena tumeongeza vifaa vingine karibuni. Pia benchi la ufundi liliandaa program maalum ambazo wachezaji walipewa kuhakikisha wanazifanya wakiwa mapumziko"

"Tutafanya maandalizi yetu hapa tukisubiri kilele cha wiki ya Mwananchi ambayo ni August 06. Siku hiyo tutacheza na timu bingwa kutoka nchi ambayo tutaitangaza baadae," alisema Manara

Kuhusu wiki ya Mwananchi, Manara amesema shamrashamra zitaanza rasmi August 01. Wiki ijayo Yanga pia itatambulisha jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2022/23

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’