Klabu ya Yanga leo inatarajiwa kuweka hadharani mikakati yao ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano ya ndani na michuano ya Kimataifa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema muda wa mapumziko umemalizika na sasa wanakwenda kuweka bayana mikakati yao kuelekea msimu mpya
"Ni hivi sisi hatuko kimya kama inavyoelezwa lakini tunafanya mambo yetu kulingana na mipango tuliyojiwekea. Wachezaji wetu tuliwapa mapumziko kuanzia Julai 05 ambapo tulitoa siku 10 kwa wachezaji wa ndani na siku 12 kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi"
"Likizo ilimalizika rasmi tarehe 17, wachezaji walianza kurejea Dar Julai 18 tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya, " alisema Bumbuli
Kutokana na ufinyu wa muda, Yanga huenda ikaendelea na kambi Avic Town
ADVERTISE HERE