Waliokuwa walinzi wa Yanga Paulo Godfrey 'Boxer' na Yassin Mustafa wamewaaga rasmi Yanga baada ya mikataba yao kumalizika
Wachezaji hao wote wamesajili na klabu ya Singida Big Stars iliyoweka makazi yake mkoani Singida

"Nianze kwa kushukuru club pendwa Yanga,mmekua nguzo kubwa kwenye safari yangu .Nashukuru kwa kuwa moja ya familia yenu kwa kipindi chote kilichopita..Asanteni yanga. Pia mashabiki kwa sapoti yenu," Boxer aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Nae Yassin amesema kwake ilikuwa heshima kubwa kuitumikia Yanga akiwashukuru wachezaji wenzake, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki
"Nitumie fursa hii kuwashukuru wananchi Yanga kwa kuwa pamoja nami katika kipindi chote tulichokuwa pamoja nasema Asante sana"
"Uongozi, benchi la ufundi, wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wote wa klabu hii kwa upendo. Niwatakie kila la kheri kwenye malengo ya msimu ujao"
"Najivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hii kubwa hapa nchini.Until next time Inshaallah," aliandika Yassin