Kilele cha wiki ya Mwananchi ni August 06 pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Siku kubwa ya utambulisho wa kikosi cha Yanga kuelekea msimu mpya wa ligi kuu, ligi ya mabingwa na kombe la FA pamoja na michuano mingine
Tamasha la mwaka huu huenda likafunika matamasha ya miaka mingine iliyopita
Baada ya kutwaa mataji yote ya ndani katika msimu uliopita, kwa sasa mashabiki wa Yanga wana furaha na wako tayari kwa mafanikio zaidi katika msimu ujao
Aidha usajili wa nyota mahiri kina Stephane Aziz Ki, Lazarus Kambole, Joyce Lomalisa, Gael Bigirimana na Bernard Morrison unafanya wiki ya Mwananchi kuwa tukio ambalo sio la kukosa
Mwaka huu huu tiketi zitaanza kuuzwa mapema na bila shaka mauzo yanaweza yakafungwa mapema sana
Yanga huenda ikawaalika mabingwa wa Zambia, Red Arrows kunogesha tukio hilo kubwa zaidi la kimichezo Tanzania