Wawili wa kigeni wanaachwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2022
Wawili wa kigeni wanaachwa

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema tayari uongozi umefanya uamuzi wa kuwapa mkono wa kwa heri wachezaji wawili wa kigeni

Baada ya kukamilisha usajili wa nyota watano wa kigeni, Yanga imekuwa na wachezaji 14, kanuni za usajili wa ndani zikiwalazimu kupunguza wachezaji wawili ili wabaki 12

"Tumekamilisha usajili wa wachezaji wa kigeni, lakini sasa tumekuwa na wachezaji 14, tumelazimika kuwapunguza wawili ili kukidhi kanuni zetu za usajili wa ndani"

"Tayari uamuzi umeshafanyika, taarifa rasmi itatolewa kupitia utaratibu tuliojiwekea," alisema Bumbuli

Hatma ya kambi Julai 18

Wakati huohuo, Bumbuli amesema mpaka kufikia Julai 18, wachezaji wote watakuwa wamerejea tayari kwa maandalizi ya msimu mpya

Bumbuli amesema uongozi ulitoa siku 10 za mapumziko kwa wachezaji baada ya mchezo wa wa fainali kombe la FA dhidi ya Coastal Union

"Tumepata changamoto kidogo ya ratiba, ligi ilimalizika Juni 29 lakini sisi tulikabiliwa na mchezo wa fainali ya FA, Julai 04 tulitoa mapumziko ya siku 10 kwa wachezaji tukaongeza na siku chache kwa ajili ya wale wanaosafiri nje ya nchi"

"Tunatarajia mpaka Julai 18 wachezaji wote watakuwa wamerejea na utaratibu wa kambi utafahamika. Safari hii tutakuwa makini kuhakikisha yale yaliyotokea msimu uliopita tunayaepuka. Hivyo kama tutaenda nje ya nchi au kambi itakuwa hapahapa nchini tutawafahamisha," alisema Bumbuli

Awali Yanga ilikuwa na mpango wa kwenda kuweka kambi Uturuki lakini kambi hiyo imeahirishwa kutokana na ufinyu wa muda

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’