Kikao cha kwanza cha Yanga chini ya Rais mpya mhandisi, Hersi Said kimefanyika kupendekeza kambi ya maandalizi kuelekea msimu mpya
Awali Yanga ilitarajia kuweka kambini nchini Marekani, lakini pendekezo hilo limegonga mwamba baada ya kocha Nasreddine Nabi kulikataa
Nabi ametaka litafutwe eneo la karibu ili kupata muda mwingi wa kuiandaa timu, mwenyewe akipendekeza timu kuweka kambi Karatu
Hata hivyo lipo pendekezo la timu kuweka kambi nchi ya Uturuki ambalo lilitolewa na baadhi ya viongozi wa Yanga.
Wachezaji wa Yanga wanatarajiwa kuanza kurejea jijini Dar es salaam siku ya Jumatano tayari kuelekea kambini kuanza maandalizi ya msimu mpya
Yanga itakuwa na takribani wiki tatu za kufanya maandalizi kabla ya kilele cha wiki ya Mwananchi August 06
August 13 Wananchi watafungua pazia la msimu mpya kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Simba ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa