Klabu ya Yanga bado inapambana kukamilisha usajili wa winga Saimon Msuva aliyekuwa akiitumikia Wydad Athletic ya Morocco
Yanga imepiga hatua kubwa katika harakati za kumnasa aliyewahi kuwa winga wao kati ya mwaka 2013 na 2017
Bado Msuva ana mgogoro na klabu ya Wydad Athletic na sasa Wananchi wamepiga hodi huko Wydad kuona uwezekano wa kununua mkataba wake uliobaki na mabingwa hao wa Morocco
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amefanya jitihada kubwa za kumshawishi Msuva arejee nyumbani hata kwa mkataba wa muda mfupi wakati akitafuta klabu barani Ulaya ili kulinda kiwango chake
Inafahamika Msuva bado ana ndoto ya kwenda kusakata kabumbu barani Ulaya
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amevutiwa sana na Msuva akiwataka mabosi wa Yanga wafanye kila jitihada wamsajili